1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Togo yajiandaa kwa uchaguzi muhimu wa bunge

Sylvia Mwehozi
28 Aprili 2024

Chama tawala na upinzani nchini Togo vimehitimisha kipindi cha kampeni kabla ya uchaguzi wa bunge utakaofanyika kesho Jumatatu, baada ya mageuzi tata ya kikatiba ambayo yamechochea mivutano ya kisiasa.

https://p.dw.com/p/4fGyS
Togo | Faure Gnassingbe
Rais Faure Gnassingbe wa TogoPicha: Ute Grabowsky/photothek/IMAGO

Chama tawala na upinzani nchini Togo vimehitimisha kipindi cha kampeni kabla ya uchaguzi wa bunge utakaofanyika Jumatatu, baada ya mageuzi tata ya kikatibaambayo yamechochea mivutano ya kisiasa.

Uchaguzi wa Jumatatu unafanyika baada ya wabunge mapema mwezi huu kuidhinisha mageuzi ambayo wakosoaji wa Rais Faure Gnassingbe wanadai kuwa atayatumia kupanua utawala wa familia yake wa zaidi ya miaka 50 katika taifa hilo la Afrika Magharibi.

Upinzani nchini humo, ulisusia uchaguzi uliopita wa bunge wa mwaka 2018, ukiorodhesha dosari. Wapinzani wamewarai wafuasi wao kukomesha utawala wa chama cha Gnassingbe cha UNIR. Akiwa madarakani kwa takribani miaka 20, Gnassingbe alimrithi baba yake aliyetawala kwa karibu miongo minne kabla yake, utawala ambao wakosoaji wanasema utapanua mamlaka yake kupitia mageuzi hayo.