1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Scholz amtaka Putin kuondoa wanajeshi wake Ukraine

18 Novemba 2023

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz ametoa wito kwa rais wa Urusi Vladimir Putin kuchukua hatua ya kwanza kuelekea kupata suluhisho la amani katika mzozo nchini Ukraine.

https://p.dw.com/p/4Z8JX
Olaf Scholz
Kansela wa Ujerumani Olaf ScholzPicha: Bernd von Jutrczenka/dpa/picture alliance

Scholz ameyasema hayo akiwa ziarani katika jimbo la Brandenburg la Ujerumani na kuongeza kuwa rais huyo wa Urusi anapaswa kuwaondoa wanajeshi wake Ukraine.

Soma zaidi: Kremlin: Putin yuko tayari kuzungumza na kansela Scholz wa Ujerumani

Akijibu swali kuhusu uwezekano wa kufanyika kwa mazungumzo ya amani kuhusu mzozo wa Ukraine, Scholz hata hivyo amesema kuwa hakuna dalili zozote za hilo kufanyika. Kansela Scholz kwa mara nyingine pia ameihakikishia Kyiv msaada wa Ujerumani katika kujilinda dhidi ya uvamizi wa Urusi kwa muda wote itakavyouhitaji.