1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Man City na Barca wajiweka nafasi nzuri kuelekea makundi

Lilian Mtono
26 Oktoba 2023

Mabingwa watetezi wa michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, Manchester City wameanza vyema kutetea ubingwa sambamba na Barcelona, wakiinyemelea hatua ya makundi.

https://p.dw.com/p/4Y2La
Erling Haaland akishangilia baada ya kufunga katika moja ya mechi za Ligi ya England, PL. Haaland amekiongoza kikosi cha Man City kushinda mabao 3-1 dhidi ya Young Boys katika Chamipons League
Erling Haaland akishangilia baada ya kufunga katika moja ya mechi za Ligi ya England, PL. Haaland amekiongoza kikosi cha Man City kushinda mabao 3-1 dhidi ya Young Boys katika Chamipons LeaguePicha: Dave Thompson/AP/picture alliance

Manchester City ikiongozwa na Erling Haaland ilishinda mabao 3-1 dhidi ya Young Boys na kuongoza kundi G, ikifuatiwa na RB Leipzig iliyopata ushindi dhidi ya Red Star Belgrade.

Barcelona, iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Shakhtar Donesk katika kundi H, huku Porto ikiifunga Royal Antwerp mabao 4-1.

Ushindi huu unawaongezea matumaini kwenye mechi za mwisho wa wiki, wakati Barcelona itakapokwaana na Real Madrid katika La Liga Classico na Man City dhidi ya Manchester United katika Derby ya PL.

Kylian Mbappe aliisaidia Paris Saint-Germain kutinga kileleni mwa Kundi F kwa ushindi wa 3-0 dhidi ya AC Milan, huku Newcastle ikiangukia pua kwa mara ya kwanza, kwa 1-0 dhidi ya Borussia Dortmund.