1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mei Mosi yaadhimishwa kwa maandamano Ujerumani na Ufaransa

1 Mei 2023

Wakati ulimwengu ukiadhimisha siku ya Mei Mosi, mkuu wa miungano ya wafanyakazi nchini Ujerumani Jörg Hofmann ametetea vikali haki za wafanyakazi kugoma.

https://p.dw.com/p/4QkmG
Deutschland Bundesweiter Streik im Verkehr hat begonnen | München
Picha: Lukas Barth/REUTERS

Akizungumza mjini Berlin wakati wa maandamano ya siku ya wafanyakazi, Hofmann amesema kwamba kama muungano hawatokubali hatua ya wafanyakazi kuzuiwa kugoma akisema jukumu la kugoma ni kuleta shinikizo la kiuchumi na kisiasa kwa watu.

Wajerumani mwaka huu wameshuhudia migomo katika sekta mbalimbali za umma ikiwemo sekta ya usafiri, wafanyakazi wakilalamikia nyongeza ya mishahara na mazingira bora ya kufanyia kazi.

Wafanyakazi kote duniani waadhimisha Siku ya Mei Mosi

Huko nchini Ufaransa nako, makumi kwa maelfu ya waandamanaji wamejitokeza kupinga sheria ya Rais Emmanuel Macron iliyopitishwa hivi majuzi ya kuongeza umri wa kustaafu kutoka miaka 62 hadi 64.

Mamlaka nchini Ufaransa zinategemea maandamano ya kati ya watu laki tano na laki sita kote nchini humo.