1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Austria itaanza tena kuchangia katika shirika la UNRWA

Amina Mjahid
18 Mei 2024

Wizara ya mambo ya nchi za nje ya Austria imesema itaachia fedha kwa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi Wakipalestina UNRWA zilizozuiwa kufuatia madai wafanyakazi wake walihusika na shambulizi la Oktoba 7

https://p.dw.com/p/4g1wr
 shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi Wakipalestina UNRWA
shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi Wakipalestina UNRWA Picha: Mahmoud Issa/ZUMAPRESS/picture alliance

Uamuzi huo umekuwa baada ya UNRWA kutoa mpango wa utekelezaji ili kuhakikisha kunakuwepo na uwazi, tathimini za ndani za wafanyakazi wake na kuimarisha namna wafanyakazi wake wanavyochunguzwa na kufuatiliwa.

Austria ilikuwa moja ya nchi zilizosimamisha msaada wake wa kifedha wa dola milioni 450 baada ya Israel kuwashutumu wafanyakazi 12 wa UNRWA kushiriki katika shambulio lililofanywa na Hamas lililosababisha vita vya Gaza. 

Ujerumani kuanza tena ushirikiano na shirika la Palestina UNRWA

Mwezi uliopita Ujerumani ilisema itaanzisha tena ushirikiano wake na shirika hilo kufuatia ripoti iliyoongozwa na Waziri wa zamani wa mambo ya nchi za nje wa Ufransa Catherine Colonna kuhusu juhudi za kuhakikisha shirika hilo linaendesha mambo yake bila ya kutegemea upande wowote.