1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kenya na Uganda zaafikiana kuweka kando tofauti zao

16 Mei 2024

Kenya na Uganda zimeafikiana kuweka kando tofauti zao na kuimarisha biashara ya mafuta kati ya nchi hizo mbili.

https://p.dw.com/p/4fwqF
Museveni na  Ruto
Rais wa Uganda Yoweri Museveni na Rais wa Kenya William RutoPicha: Simon Maina/AFP/Getty Images

Kenya na Uganda zimeafikiana kuweka kando tofauti zao na kuimarisha biashara ya mafuta kati ya nchi hizo mbili.

Matiafa hayo  yamekubaliana kujenga bomba la mafuta kutoka Eldoret hadi Kampala na pia kusafirisha bidhaa hiyo moja kwa moja kupitia Nairobi.

Makubaliano haya yanajiri katika ziara rasmi ya Rais Yoweri Museveni nchini Kenya inayodhamiria kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia.

Soma;Samia, Museveni na Ruto wakutana kujadili EAC na Uchumi

Kwenye mkutano wa pamoja na waandishi wa habari, Rais Museveni alibainisha kuwa udugu wa Uganda na Kenya ni muhimu hasa kwenye masuala ya ushirikiano wa biashara kauli iliyoungwa mkono na mwenyeji wake wa Kenya rais William Ruto.