1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Mwendesha mashtaka ICC aomba waranti dhidi ya Netanyahu

Amina Mjahid
20 Mei 2024

Mwendesha mashitaka wa ICC ameomba warranti wa kukukamatwa Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, Waziri wake wa ulinzi Yoav Gallant na viongozi watatu wa Hamas kufuatia madai kuhusika na uhalifu wa kivita.

https://p.dw.com/p/4g4r9
Mwendesha Mashtaka Mkuu wa ICC, Karim Khan
Mwendesha Mashtaka Mkuu wa ICC, Karim Khan Picha: Chepa Beltran/LongVisual via ZUMA Press/picture alliance

Mwendesha mashitaka wa Mahakama ya kimataifa inayoshughulikia kesi za uhalifu wa kivita ICC Karim Khan, amesema ameomba warranti wa kukukamatwa Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, Waziri wake wa ulinzi Yoav Gallant na viongozi watatu wa kundi la wanamgambo la Hamas kufuatia madai kuhusika na uhalifu wa kivita.

Khan amesema katika taarifa iliyotolewa wakati vita hivyo vikiendelea kwa miezi saba sasa, kwamba ana ushahidi unaoonesha kwamba wahusika wote wamehusika katika uhalifu huo wa kivita na uhalifu dhidi ya binaadamu.

Soma pia: ICC yaonya dhidi vitisho vya ulipizaji kisasi kwa watendaji wake

"Ofisi yangu inaushahidi unaoonesha kuwa watu hawa kupitia mpango wa pamoja wamewanyima watu wa Gaza vitu muhimu vya kuwafanya binaadamu waendelee kuishi. tumefikia uamuzi huo kufuatia watu tuliowahoji ambao ni waathiriwa, watu walioshuhudia vita hivyo pamoja na wataalamu," alisema Khan.

Viongozi wa Hamas Yahya Sinwar, Mohammed Al-Masri, kiongozi wa kijeshi wa kundi hilo pamoja na Ismail Haniyeh, ambaye ndio Mkuu wa kundi hilo pia huenda wakakamatwa kufuatia Uhalifu uliotekelezwa Katika vita hivyo.

Khan amesema  majaji wa kesi hiyo ndio watakaoamua kama ushaidi uliopo unatoasha kutoa hati za kuwakata viongozi hao. Hata hivyo viongozi wote wa Israel na Palestina wamekanusha kuhusika na uhalifu huo.