1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa Somalia anaongoza kikao cha mkutano wa kilele

Saumu Mwasimba
14 Mei 2024

Rais Hassan Sheikh Mohamud wa Somalia leo ataongoza mkutano kati ya serikali kuu na viongozi wa serikali za majimbo ambao unatarajiwa kujadili juu ya mabadiliko ya katiba yanayosababisha mvutano pamoja na vita.

https://p.dw.com/p/4fqF2
Rais Hassan Sheikh Mohamud
Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud akizungumza wakati wa Kikao cha 37 cha Kawaida cha Umoja wa Afrika (AU) mjini Addis Ababa, Ethiopia Februari 17,Picha: REUTERS

Viongozi wa majimbo ya kusini magharibi ya Jubaland na Galmudug wameshawasili mjini Mogadishu kushiriki mkutano huo wa kilele wa kitaifa ambao awali ulikuwa umepangwa kuandaliwa Aprili 20 lakini ukaakhirishwa kufuatia mivutano ya kisiasa iliyozuka kuhusu mageuzi ya sheria za nchi. Bado haijafahamika ikiwa viongozi wa majimbo ya Hirshabelle na Puntland watashiriki. Majimbo hayo yanatajwa kusitisha ushirikiano na serikali kuu  kupinga mageuzi ya katiba. Mkutano huo pia utajadili kuhusu mvutano wa hivi karibuni kati ya Somalia na jirani yake Ethiopia. Kadhalika mkutano huo umeandaliwa katika wakati ambapo rais Mohamud kesho anaadhimisha miaka miwili tangu alipoingia madarakani.