1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMyanmar

Jumuiya ya Kimataifa yapaswa kutafakari kuhusu Myanamar

Tatu Karema
21 Juni 2023

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya haki za binadamu nchini Myanmar Thomas Andrews, amesema Jumuiya Kimataifa inapaswa kutafakari mwelekeo wake katika mgogoro wa Myanamar.

https://p.dw.com/p/4SskB
Min Aung Hlaing
Picha: AP/picture alliance

Akizungumza huko Jakarta Indonesia, amebaini kwamba hakuna utekelezwaji wowote uliofanyika wa mpango wa amani wa vipengele vitano wa jumuiya ya ushirikiano wa kiuchumi na usalama wa  nchi za kusini Mashariki mwa Asia, SEAN,nchini Myanmar.

Mpango huo uliofikiwa na utawala wa kijeshi wa Myanmar

Mpango huo uliofikiwa na utawala wa kijeshi wa Myanmar baada ya kutwaa madaraka kwa nguvu kupitia mapinduzi mwaka 2021,ulitaka usitishwaji wa vita mara moja,kufunguliwa njia za kupelekwa msaada wa kibinadamu,pamoja na kuanzishwa mazungumzo yatakayojumuisha pande zote kutafuta amani nchini humo.

Utawala wa kijeshi haupaswi kualikiwa katika mikutano ya kidiplomasia

Mjumbe huyo wa Umoja wa Mataifa pia amesena  Jumuiya ya ASEAN haipaswi kuwaalika viongozi wa utawala wa kijeshi kwenye mikutano ya ngazi za juu ya kidiplomasia,vinginevyo utaingia kwenye hatari ya kurudi nyuma kwa kuuhalalisha utawala huo wa kijeshi.