1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu 190 wamenusurika kwa ajali ya ndege nchini Uturuki

Sudi Mnette
9 Mei 2024

Jumla ya watu 190 wamenusurika nchini Uturuki baada ya ndege walikuwamo kupasuka tairi wakati wa kutua katika uwanja wa ndege wa wa Gazipasa. Wizara ya usafirishaji Uturuki imesema hakuna aliyejeruhiwa.

https://p.dw.com/p/4fg8L
Ndege ya mizigo ya kampuni ya kusafirisha mizigo ya FedEx Express
Ndege ya mizigo ya kampuni ya kusafirisha mizigo ya FedEx Express Picha: Julia Nikhinson/REUTERS

Kampuni yenye uratibu wa safari wa ndege hiyo aina ya Boing 737-800 ya shirika la ndege la Corendon la hukohuko Uturuki, imesema pamoja na tatizo hilo ndege ilifanikiwa kusimama uwanjani.

Ndege, ilikuwa na abiria 184 na wafanyakazi sita, ikitokea Cologne, Ujerumani. Shirika Corendon limekanusha ripoti za vyombo vya habari vya Uturuki kuwa ndege hiyo ilikuwa ikitua kwa kutanguliza eneo la mbele, yaani pua yake. 

Soma pia: Polisi ya Uturuki yawatia mbaroni waandamanaji 200

Katika tukio lingine la jana Jumatano ndege ya mizigo ya Boeing 767 mali ya kampuni ya kusafirisha mizigo ya FedEx Express ilitua kwa dharura katika Uwanja wa Ndege wa Istanbul baada ya gia kushindwa kufanya kazi. Na kadhalika katika mkasa huo hakuna aliyejeruhiwa na wahudumu waliweza kufanya uokozi wa ndege hiyo salama.