1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Gallant: Israel itashinda malengo yake ya kivita Gaza

Sudi Mnette
9 Mei 2024

Waziri wa Ulinzi wa Israel Yoav Gallant amewaambia "maadui na marafiki" wa taifa lake kwamba watafanya kinachostahili kufikia malengo ya vita Gaza, ikiwa ni jibu kwa Marekani iliyotaka isitishe operesheni huko Rafah.

https://p.dw.com/p/4fgA6
Israel, Tel Aviv | Waziri wa Ulinzi wa Yoav Gallant akiwa na maafisa wa jeshi.
Waziri wa Ulinzi wa Israel Yoav Gallant akiwa na maafisa wa jeshi.Picha: Israeli Ministry of Defense/Handout/Anadolu/picture alliance

Kauli hiyo aliyoitoa katika hafla ya kuwakumbuka waliouwawa katika vita vya Israel, inafuatia onyo la Rais Joe Biden, akisema kwamba Marekani itasitisha utoaji wa silaha kwa Israel kama taifa hilo litaendelea na mashambulizi yake katika eneo la Rafah, eneo ambalo zaidi ya Wapalestina milioni moja walioachwa bila ya makazi, wanajipatia hifadhi.

Soma pia:Meli ya shehena ya misaada yang'oa nanga Cyprus kuenda Gaza

Kwa mujibu wa taarifa ambayo imetolewa na ofisi yake, Waziri Gallant amesema wataendelea kuwa madhubuti, watafanikisha malengo yao, watayashambulia makundi ya Hamas na Hezbollah na kufanikisha lengo la kiusalama.

Vifaru vya Israel vilichukua udhibiti wa upande wa Palestina wa kivuko cha mpaka cha Rafah na Misri mapema juma hili na vinaelezwa kuwa karibu na viunga vya mji wa karibu wa Rafah.